Kuhusu Mwandishi: Padre Karugendo:

Padre Privatus Karugendo (58), alikuwa Padre wa Kanisa Katoliki la Rulenge, ambalo siku hizi linaitwa Rulenge-Ngara, hadi mwaka 2000. Read More
 

DIBAJI

... Nimefarijika kuyasoma mazungumzo baina ya Padri Privatus Karugendo na Ndugu January Makamba, mmoja wa viongozi mahiri wa zama za sasa. Nawapongeza kwa kuamua kuyaweka mazungumzo yao katika rekodi ya maandishi. Hakika tumejifunza mengi kuhusu na kutokana na historia na falsafa ya maisha ya Ndugu Makamba pamoja na fikra zake kuhusu Tanzania ijayo.

Jamii inanufaika tunapowafahamu kwa kina viongozi wetu. Utaratibu huu wa Padri Karugendo ni jambo jema na inabidi uendelezwe. Binafsi nilikuwa namfahamu Ndugu Makamba kama kiongozi ndani ya Chama chetu na kwenye Serikali. Fursa ya kusoma mazungumzo yake imenisaidia kumfahamu zaidi kama mtu lakini pia kufahamu fikra zake. Nimefarijika kwamba nchi yetu na Rais wetu Kikwete ameendeleza utamaduni aliouanzisha Mwalimu Nyerere na kuendelezwa nami wa kuwaamini vijana na kuwapa fursa za uongozi ili kuwaandaa kuiongoza nchi yetu. Nilimteua Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete

Kila zama na kitabu chake, kila zama na changamoto zake na kila zama na mitume wake. Wenye zama zao wanakitendea haki kizazi chao na vizazi vijavyo wanaporekodi masaibu na matumaini ya zama husika. Nimejifunza kupitia mazungumzo haya kuhusu aina ya Tanzania ambayo Ndugu Makamba anaitaka. Imani yangu ni kwamba mazungumzo haya, pamoja na mengine ambayo wengine watayafanya, yataleta mjadala wenye afya kuhusu Tanzania tuitakayo.

Ali Hassan Mwinyi
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dar es Salaam
22/12/2014

 

Utangulizi:

Kitabu hiki ni matokeo ya mahojiano yetu na Mheshimiwa January Makamba. Hatukuwa kabisa na lengo la kuandika kitabu, bali ilikuwa ni kiu ya kutaka kumfahamu huyu kijana, Mbunge na Naibu Waziri ni nani, ana fikra na ndoto gani kuhusu Tanzania tuitakayo? Read More


Maswali na Majibu

 

1. Kabla hatujaanza, na kabla sijasahau, nimekuwa na hamu kubwa ya kusikia kauli yako mwenyewe kuhusu hili suala la Urais. Mjadala wa Urais, hasa ndani ya Chama chenu, umekuwa mkali sana. Majina mengi yametajwa, ikiwemo lako. Je, ni kweli unaingia? Nimekusikia ukisema umefikia uamuzi wa kugombea kwa asilimia 90. Hiyo asilimia 10 bado tu?

  

Jibu namba. 1   ...

Issakwisa Mwakisambwe         2015-06-08 15:16:58

ccm hamuwezi kutoa mgombea msafi anayeweza kutekeleza muyasemayo nyie watia nia kwani misingi ya chama chenu ni wizi,ujangili,ufisadi ccm ndio kwenu hata hamuwezi kufanikisha muyasemayo .kwaujumla hakuna mgombea ccm anayeweza kutujengea Tz mpya
...

Lebai Nsemwa         2015-06-07 19:24:41

Kila la kheri Makamba katika kuusaka urais. Kutokana na jibu kwa swali la kwanza ni dhahiri unauwezo wa kuwa rais wetu kupitia CCM.
...

Priscus Buretta         2015-01-18 21:08:18

...

Gadaf Felix         2015-01-18 20:41:26

NDIyo
...

Ruda         2015-01-16 17:42:23

Ni Kweli?
 

2. Naamini watu wengi watapenda kujua January Makamba ni nani haswa. Hebu tuelezee kwa kifupi historia yako; ulizaliwa wapi, umekulia wapi, umepitia wapi, umefikaje hapa ulipo leo? Jina la baba yako limekubeba?

  

Jibu namba. 2   ...

Hassani Juma Shabani         2015-01-29 16:50:30

Nimejifunza kitu hapo Safi sana kiongozi
...

Benjamin Langeni Mndeme         2015-01-22 10:36:37

safi CV nzuri inaridhisha
...

Muya K Alli         2015-01-19 16:58:38

hongera rais ajaye
...

Marwaa Marwaa         2015-01-19 12:39:52

historia nzuri, wewe ni shujaa
...

Amon Furela         2015-01-16 20:16:23

nimefurahi sana kuona unavoijua vizuri geographia yamkoa wetu wakagera tunahitaji kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha unapata uhongoz wajuu.
 

3. Je umeshapata watoto? Kama ni ndiyo ni wangapi? Je, mtazamo wako kuhusu familia na malezi ya watoto ni upi? Watu wanasema maji hufuata mkondo, je, ungependa watoto wako wawe wanasiasa kama wewe?

  

Jibu namba. 3   ...

Muya K Alli         2015-01-19 17:01:06

vizuri
 

4. Umesema kwamba ulisomea Chuo Kikuu cha Kikatoliki Marekani. Kama ujuavyo, mimi ni Padre. Napenda kusikia kidogo kuhusu suala hili. Ulijifunza nini pale.

  

Jibu namba. 4   ...

Marwaa Marwaa         2015-01-18 12:29:39

Ni vema
...

Marwaa Marwaa         2015-01-18 12:29:39

Ni vema
...

Marwaa Marwaa         2015-01-18 12:29:39

Ni vema
...

Marwaa Marwaa         2015-01-18 12:29:37

Ni vema
 

5. Umenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari ukisema kwamba sasa ni wakati wa viongozi vijana kujitokeza na kuchua nafasi kubwa za uongozi kama Urais wa nchi. Kwa nini mjadala huu ni muhimu wakati huu na vitu gani vipya vya kuibadilisha Tanzania vinavyoweza kufanywa na vijana na si wazee? Kwanini vijana waaminiwe kwenye nafasi kubwa wakati hawana uzoefu wa kuongoza?

  

Jibu namba. 5   ...

Athman Mchujuko         2015-06-08 05:07:04

Safi sana January. Umeelezea vizuri sana suala la umri. Umri si Tija kabisa katika uongozi. Watanzania wengi bado wana mawazo ya kusema kwamba kiongozi lazima awe mzee. Mimi nakubaliana na wewe 100 percent. Rais Obama kachukua nchi akiwa na miaka 46. Kuna
...

Msukuma Mzanaki         2015-01-22 13:19:34

wazee wametupatia uhuru, baada ya miaka 50 imefika wakati tuwasaidie katika matatizo ya maji, umeme, afya, miundo mbinu, ustawi wa jamii na elimu na kupinga kwa asilimia 110 RUSHWA..
...

Amon Furela         2015-01-16 20:12:15

sasaiv inchi hii inataka viongozi vijana mda wawazee umekwisha,weneed change
 

6. Je, umekomaa vya kutosha kushika nafasi ya Urais? Umefanya nini kwenye wizara yako, kiasi kwamba watu waweze kuamini kwamba unastahili nafasi ya juu zaidi ya hiyo uliyo nayo kwa sasa? Ulipochaguliwa kuwa Mbunge ulianzisha Shirika la Maendeleo Bumbuli. Nini kilikusukuma? Shirika linafanya nini na limewasaidia vipi watu wa Bumbuli. Je, kama jimbo bado lina changamoto unastahili kuomba nafasi ya juu?

  

Jibu namba. 6   Hakuna Maoni
 

7. Ni changamoto gani kubwa zinawakabili vijana wa Tanzania? Wanasiasa wengi wamekuwa wakisema watamaliza tatizo la ajira nchini. Kuna mawazo gani mapya kutoka kwa viongozi wa kizazi kipya ya kumaliza tatizo hili?

  

Jibu namba. 7   Hakuna Maoni
 

8. Kuna wazo kwamba nchi tukiigawa katika majimbo ya kiutawala, itapiga hatua za kimaendeleo kwa haraka. Kuna siku nilikusikia ukipinga wazo hili na ukasema kwamba badala ya majimbo ya kiutawala tuigawe nchi kwenye majimbo ya kiuchumi. Je, unaweza kufafanua fikra hizi?

  

Jibu namba. 8   Hakuna Maoni
 

9. Baada ya kuingia Bungeni, ulipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati nyeti ya Nishati na Madini. Kwanza, tuambie uliwezaje kupata Uenyekiti wa Kamati nyeti katika wiki chache tu baada ya kuingia Bungeni. Tuelezee baadhi ya changamoto kwenye nafasi hii, lakini pia mlichukua hatua gani kulisaidia taifa kwenye sekta hizi nyeti? Ilikuwaje Kamati hii ikavunjwa mara tu baada ya wewe kuachia Uenyekiti? Nini kifanyike kumaliza tatizo la mgao wa umeme na bei kubwa za umeme?

  

Jibu namba. 9   Hakuna Maoni
 

10. Umeeleza kwamba ulikuwa sehemu ya kampeni ya Urais ya CCM mwaka 2005 na kwamba ulipata nafasi ya kuzunguka na Mheshimiwa Kikwete akiwa mgombea wa Urais wa CCM kwenye uchaguzi huo. Ulikuwa unafanya shughuli gani na ulijifunza nini katika shughuli ile?

  

Jibu namba. 10   Hakuna Maoni
 

11. Kwa miaka mitano na zaidi, ulipata nafasi ya pekee ya kuwa karibu na Rais wakati wote. Kutokana na nafasi hiyo ni mambo gani ya msingi uliyojifunza na yakakujenga kuwa kama ulivyo leo hii? Kwa nini uliamua kuacha kazi nzuri ya Ikulu na kwenda kugombea ubunge? Je, ilikuwa rahisi Rais kukuachia?

  

Jibu namba. 11   Hakuna Maoni
 

12. Hivi karibuni wananchi wengi hasa wa kipato cha chini na cha kati wamekuwa wakilalamika kwamba maisha yamekuwa makali, na gharama za maisha zimekuwa zikipanda kila kukicha. Maarifa gani yanahitajika ili kuweza kupunguza ukali wa maisha kwa Watanzania?

  

Jibu namba. 12   Hakuna Maoni
 

13. Watanzania wengi wanajishughulisha na kilimo, ufugaji na uvuvi lakini wamekuwa hawanufaiki na shughuli hizi licha ya mipango mingi tangu wakati wa uhuru hadi sasa. Je, kizazi kipya cha uongozi wa nchi kinapaswa kuwa na maarifa gani mapya kuhusu mapinduzi ya kilimo na maendeleo ya uvuvi na ufugaji?

  

Jibu namba. 13   Hakuna Maoni
 

14. Tanzania imekuwa ikisifika kwamba uchumi wake unakua kwa kasi kwa miaka kadhaa sasa. Lakini wananchi wengi bado hawajaona hayo manufaa. Nini kifanyike wananchi nao waone na wanufaike na uchumi kukua? Unauelezeaje uchumi wetu kwa ujumla?

  

Jibu namba. 14   Hakuna Maoni
 

15. Mwaka jana nilisoma kwenye vyombo vya habari kwamba ulipata tuzo ya taasisi ya National Democratic Institute ya Marekani, unaweza kutueleza ni tuzo ya nini na kwa nini uliipata? Pili, tulisoma kwamba uliteuliwa na taasisi ya World Economic Forum kuwa mmoja wa viongozi vijana mashuhuri duniani (Young Global Leaders). Pia tena majuzi tukasoma kwamba jarida mashuhuri duniani la Forbes limekutaja kuwa mmoja wa watu kumi wenye ushawishi Afrika kwa mwaka 2014. Ni kwanini unadhani wanakupa hizi tuzo? Na je, tuzo hizi zina maana gani kwa wapiga kura wako?

  

Jibu namba. 15   Hakuna Maoni
 

16. Kama kiongozi kijana uliyepata kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ikulu, unazungumziaje nafasi ya Tanzania katika siasa za kimataifa?

  

Jibu namba. 16   Hakuna Maoni
 

17. Tunaona jinsi nchi jirani zetu wanavyopata changamoto za usalama. Je, sisi tufanyaje kuepukana nazo?

  

Jibu namba. 17   ...

Marwaa Marwaa         2015-01-19 09:21:44

safi sana, usalama ni muhimu kwetu
 

18. Kiwango cha elimu katika taifa letu kimeporomoka, ni kwa nini na unafikiri ni kitu gani kifanyike kuinua hali ya elimu katika taifa letu?

  

Jibu namba. 18   Hakuna Maoni
 

19. Walimu ni sehemu kubwa ya watumishi wa umma. Je, wewe unayajua matatizo yao? Una fikra na mawazo gani ya kuyashughulikia? Vipi kuhusu wahadhiri wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu?

  

Jibu namba. 19   Hakuna Maoni
 

20. Kumekuwa na malalamiko kuhusu utendaji Serikalini, hasa juu ya urasimu; kwamba maamuzi hayafanyiki kwa wakati, lakini pia hakuna uwajibikaji. Je, nini kifanyike kurekebisha hali hii?

  

Jibu namba. 20   Hakuna Maoni
 

21. Wananchi wanalalamikia sana ufisadi. Mikakati ya sasa inaelekea haijafanikiwa kiasi cha kuridhisha wananchi. Je, wewe una mbinu zozote mpya za kupambana na tatizo hili? Je, unaongeleaje ufisadi wa Richmond, EPA na IPTL.

  

Jibu namba. 21   ...

Amon Furela         2015-02-02 20:51:30

je?unao ujasiri wakutoa mahamuz yakupambana naufisadi wakati wanafanya ufisadi niwatu waCCM ambao hoa ndo wanaoweza kukuweka madarakani?
 

22. Kumekuwa na hii dhana ya kufanya maamuzi magumu kama sifa ya uongozi. Je, unalisemeaje hili? Je, wewe umeshawahi kufanya maamuzi yoyote magumu kwenye uongozi wako?

  

Jibu namba. 22   Hakuna Maoni
 

23. Hapa tupo Dar es Salaam. Inaelekea karibu kila mtu anataka kuhamia na kuishi Dar es Salaam. Una maoni gani kuhusu nafasi ya Jiji la Dar es Salaam katika maendeleo ya nchi yetu? Nini changamoto za jiji hili na nini kifanyike kuzirekebisha?

  

Jibu namba. 23   Hakuna Maoni
 

24. Mwaka 2012 ulipeleka Bungeni Muswada Binafsi wa Sheria ya Kudhibiti shughuli za Upangishaji Nyumba. Tuelezee maudhui yake, nini kilikusukuma na muswada huo umefikia wapi

  

Jibu namba. 24   Hakuna Maoni
 

25. Inaelekea siku hizi kila mwanasiasa anajikita katika kundi la vijana na kuzungumzia masuala yanayowavutia vijana. Hakuna makundi mengine ya kuyasemea? Ni makundi gani na mahitaji yao ni yapi na ufumbuzi wa changamoto zao ni upi?

  

Jibu namba. 25   Hakuna Maoni
 

26. Umekuwa mmoja ya viongozi ambao wanaliongelea sana suala la mabadiliko ya kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watu nchini na taifa kuwa changa kiumri. Unaweza kutuelezea kwa upana nini maana ya mabadiliko haya kwenye mustakabali wa taifa letu la leo na la kesho?

  

Jibu namba. 26   Hakuna Maoni
 

27. Miaka ya hivi karibuni imejitokeza dalili kwamba mahusiano ya watanzania wenye dini tofauti si mazuri na kuna dalili kwamba hali hii inaweza kuleta kutoelewana siku za usoni. Wewe unalisemeaje suala hili? Nini nafasi ya imani ya kiroho katika kumwongoza Kiongozi wa nchi?

  

Jibu namba. 27   Hakuna Maoni
 

28. Wewe kama kiongozi kijana, umewasaidiaje hawa vijana wenzenu wa Bongo Movies na vijana wa muziki wa kizazi kipya maana yake kila siku wanalalamika. Pia inaelekea tumetelekeza maendeleo ya sanaa kwa ujumla. Tufanyeje?

  

Jibu namba. 28   ...

Mohamed         2015-01-20 01:04:45

Hapa Sanaa ni pamoja Ya kuenzi historia ya nchi yetu majina Ya kihistoria yatumike kwenye vituo vipya vya mabadiliko na kwengineko kuenzi historia Ya nchi yetu
 

29. Tanzania imekuwa ikijulikana kama kichwa cha mwendawazimu kwenye medani ya michezo ya kimataifa. Ni muda mrefu sasa tumeshindwa kupata medali zozote kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola au Olimpiki. Mara ya mwisho kwa Taifa Stars kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Afrika ilikuwa ni miaka 36 iliyopita. Una fikra gani mpya katika kulirekebisha hili na kuwafanya Watanzania kujisikia fahari kutokana na mafanikio ya wanamichezo wake?

  

Jibu namba. 29   ...

Mohamed         2015-01-20 01:20:34

Hapa tuangalie namna ya kuwatumia wazawa kina lunyamila, masatu nk Hawa wanafaa kuwa makocha Bora tuwape nafasi
 

30. Watu wengi wamekuwa wanalalamikia bandari na reli. Wengine wanasema kwamba kwa takribani miaka kumi sasa bandari na reli ziko vilevile, hakuna upanuzi wala ujenzi mpya. Una maoni gani kuhusu miundombinu ya usafirishaji? Nini kipya kinaweza kufanyika

  

Jibu namba. 30   Hakuna Maoni
 

31. Nimetembea sana vijijini na nimeona kuwa vijiji vingi havina huduma yoyote ya afya. Hata kule ambapo zipo watumishi hawatoshi, vifaa hakuna, hakuna umeme, na wakati wote hakuna dawa. Ukienda hospitali, iwe ndogo au kubwa, una hatari ya kupata ugonjwa kuliko nyumbani. Haya matatizo wewe unayaonaje? Kwa kweli watu hawamudu gharama za matibabu na wanakufa bila sababu za msingi. Nini kifanyike?

  

Jibu namba. 31   Hakuna Maoni
 

32. Umesema kwamba Rais Kikwete amejitahidi kuboresha huduma. Unadhani ni huduma gani ya jamii bado ni kero kwa Watanzania na unadhani kuna maarifa gani mapya ya kuitatua?

  

Jibu namba. 32   Hakuna Maoni
 

33. Ukiwa kama kiongozi kijana wa CCM, uliyepata fursa ya kuwa kiongozi wa juu wa Chama chenu, huoni kama Chama chenu kimepoteza mwelekeo na kinapata ushindani mkubwa sasa? Kuna sababu za Chama chenu kuendelea kuaminiwa na Watanzania? Ukichaguliwa Rais, pia unakuwa Mwenyekiti wa CCM, je kijana anaweza kukiongoza Chama kikongwe kama CCM?

  

Jibu namba. 33   Hakuna Maoni
 

34. Hapa Tanzania karibu kila mtu, hata ambao ni watumishi wa Serikali na hata wananchi wa vijijini ni wajasiriamali. Lakini ujasiriamali unakwamishwa na ukosefu wa mikopo. Benki ziko nyingi lakini hazikopeshi watu maskini ambao hawana dhamana. Taasisi za ukopeshaji, microfinance, zimejaa lakini riba ni kubwa na watu wanashindwa. Kulikuwa na Mabilioni ya JK lakini hayakufika mbali. Kuna jambo gani kubwa na jipya la kumaliza tatizo hili?

  

Jibu namba. 34   ...

Mohamed         2015-01-20 14:59:33

Kaka kama hizi ni ahadi Zako Basi uwe na pesa Sio mzaha maana miradi hiiii ni mikubwa Bado wananchi wengi Hawana elimu Ya ujasiriamali ubunifu ila ni mawazo poa
 

35. Nini nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari katika kuchochea maendeleo ya taifa letu. Unaongeleaje suala la kuwa na vyombo vya habari vingi ambavyo vinaandika habari za uchochezi.

  

Jibu namba. 35   ...

Mohamed         2015-01-20 15:14:16

Hapa Kweli uzalendo Bado mdogo Sana kama magazeti yanaripoti kuwepo kwa Ebola Tz bila ya udhibitisho Jambo kama hilo kinachafua nchi
 

36. Baada ya uvumbuzi wa gesi nchini, kumekuwa na mjadala kuhusu Watanzania kunufaika na rasilimali za taifa hili. Una maoni gani kuhusu huu mjadala? Nini kifanyike ili watu wa hali ya chini wanufaike? Kama kiongozi umeshiriki vipi kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali zao?

  

Jibu namba. 36   Hakuna Maoni
 

37. Wakati wa Bajeti, kila tunapozungumzia kutotekelezwa kwa miradi ya maendeleo, kutolipwa kwa wazabuni, kutolipwa kwa walimu na askari, tunasikia sana msemo wa kasungura kadogo. Je, kutokana na hali hii, kuna matumaini ya kupata maendeleo kama kila wakati Serikali inasema haina fedha ya kutekeleza majukumu yake ya msingi? Je, kuna maarifa gani mapya, ambayo wewe kama kiongozi wa kizazi kipya, ambayo unayo kuhusu namna ya kupata fedha za maendeleo?

  

Jibu namba. 37   Hakuna Maoni
 

38. Mwaka jana niliona picha yako kwenye gazeti ukiwa Butiama na Mama Maria Nyerere mkiomba pembeni ya kaburi la Mwalimu Nyerere. Ulifikaje huko? Mama Maria alikupa usia gani? Unazungumziaje nafasi ya Mwalimu Nyerere kwenye siasa za sasa za nchi yetu?

  

Jibu namba. 38   Hakuna Maoni
 

39. Je, kati ya marais wanne waliowahi kuliongoza taifa letu, unafikiri ni rais gani ameacha historia kubwa kama Rais aliyefanya mambo makubwa kuliko wote katika taifa letu?

  

Jibu namba. 39   Hakuna Maoni
 

40. Kuna mambo yoyote unayodhani hatukuyazungumzia ambayo unadhani yana umuhimu katika ustawi wa nchi yetu?

  

Jibu namba. 40   Hakuna Maoni
 

Matukio katika Picha/Video

Hakuna Picha zilizo pakiwa wakati huu

Video zilizopakiwa

Hakuna Video zilizo pakiwa wakati huu
Hakuna Audio zilizo pakiwa wakati huu